MASUALA KUMI YANAYOJITOKEZA MARA KWA MARA KUHUSU TAKWIMU YA ASASI ZA KIRAIA ZANZIBAR

1. Nini maana ya Takwimu ya Asasi za kiraia Zanzibar?
2. Asasi zipi za kiraia zinaingizwa katika Takwimu hii?
3. Nini umuhimu wa Takwimu hii kimaendeleo ya jamii ya Zanzibar?
4. Nani Mmiliki wa Takwimu hii na Je Inahitaji kulipia kupata taarifa?
5. Ni Faida gani zinapatikana Jumuia yetu ikiingizwa katika Takwimu hii?
6. Jumuia yetu ifanyeje ili iweze kuoredheshwa katika Takwimu hii?
7. Je iwapo sina huduma ya mtandao naweza kupata taarifa ya Takwimu hii?
8. Je Jumuiya yetu itafutiwa usajili ikiwa haimo katika Takwimu hii?
9. Jee yawezekana kurekebisha taarifa zilizoingizwa kwenye Takwimu hii?
10. Jee Takwimu hii ni mbadala wa Serikali wa kusajili Jumuiya za Kiraia?

1. Nini maana ya Takwimu ya Asasi za kiraia Zanzibar?

Ni orodha ya Asasi za kiraia ambazo zinazofanyakazi Zanzibar, Zinafanya kazi gani, Wapi zimejikita shughuli zao, Ni nani viongozi wao, na ni yapi mafanikio yao makuu katika kipindi cha miaka mitano.

2. Asasi zipi za kiraia zinaingizwa katika Takwimu hii?

Jumuia zinazojiendeleza,vikundi vya kidini,vikundi vya wanawake,jumuia za kitaifa na za kimataifa jamii za kitaalamu ambazo zimesajiliwa chini ya kifungu cha sheria No. 6 ya Zanzibar.

3. Nini umuhimu wa Takwimu hii kimaendeleo ya jamii ya Zanzibar?

Inatoa habari/taarifa juu ya:- Asasi ziliopo, zinafanya nini,wapi zilipo, Vyanzo vyao vya fedha na vilevile muelekeo wa juhudi zao. Hii inawezesha mashirika mengine katka kujitolea na kujishirikisha vyema kikazi na Asasi za Kiraia.

4. Nani Mmiliki wa Takwimu hii na Je Inahitaji kulipia kupata taarifa?

Takwimu hii ni mali ya Wizara ya Katiba na Utawala Bora - Zanzibar na hutolewa bila ya malipo kwa wanaharakati wa maendeleo wenye shauku ya kufanya kazi na Asasi hizo za kiraia Zanzibar. Kinachotakiwa kufanyika kwa watumiaji ni kukiarifu kitengo cha Asasi za kiraia (The NGO Coordination Unit) na Kituo cha Kulelea Asasi za Kiraia pindipo wakitaka kunakili/kuchapisha yaliyomo katika Takwimu hii.

5. Ni Faida gani zinapatikana Jumuia yetu ikiingizwa katika Takwimu hii?

Taarifa za mafanikio yako na mahitaji yako ya fedha zitawafikia wadau wengi ambao wanaweza kutaka kushirikiana nawe katika maendeleo. La msingi ni kuzielezea vizuri kazi zenu ili wale wadau muhimu wa maendeleo waweze kupata taarifa hizo.

6. Jumuia yetu ifanyeje ili iweze kuoredheshwa katika Takwimu hii?

Ni kazi rahisi unachotakiwa ni kujaza fomu na kuiwasilisha kwa mujibu wa maelezo yake katika mtandao. Namna nyingine ni kuchapisha na kuijaza fomu iliopo kwenye mtandao na kuipeleka katika Ofisi za karibu za Wizara ya Katiba na Utawala Bora au Makao Makuu yake yaliopo Mjini Zanzibar.

7. Je iwapo sina huduma ya mtandao naweza kupata taarifa ya Takwimu hii?

Huduma hii ya Takwimu inapatikana pia katika njia mbili zaidi ya ile ya internet-Kwa njia ya CD ROM na Vitabu. Njia zote mbili hizi waweza kuzipata katika Ofisi za idara ya Asasi za kiraia,Ofisi za Kituo Cha Kulelea Asasi za Kiraia kiliopo Mji Mkongwe,ANGOZA -Unguja na Ofisi za PACSO zilipo Pemba.

8. Je Jumuiya yetu itafutiwa usajili ikiwa haimo katika Takwimu hii?

Takwimu hii si mbadala wa Utaratibu Rasmi wa Usajili kwa Msajili wa Asasi za Kiraia au katika Ofisi za Wizara ya Kazi,Wanawake,Vijana na Maendeleo ya Watoto. Jumuiya ambazo zitaingizwa katika Takwimu hii ni zile ambazo zimesajiliwa tu.

9. Jee yawezekana kurekebisha taarifa zilizoingizwa kwenye Takwimu hii?

NDIO. Yawezekana hasa pale likigundulika tatizo au iwapo kuna taarifa ya nyongeza iliyothibishwa na Uongozi wa Juu ,basi taarifa hii itaingizwa katika takwimu hii.

10. Jee Takwimu hii ni mbadala wa Serikali wa kusajili Jumuiya za Kiraia?

HAPANA. Takwimu hii ni huduma ambayo Kitengo (cha Wizara) cha Jumuiya Zisizokuwa za Kiserikali hupewa ili kupata taarifa sahihi za Jumuiya zisizokuwa za Kiserikali zilizohai,zilizolegelege na zilizokufa ukilinganisha na orodha ndefu iliopo ya Jumuiya hizo.