Maelekezo kwa Jumuiya za Kizanzibari
Lengo mahsusi la kutengeneza Mradi huu wa Takwimu ya Jumuiya za Kiraia Zanzibar ni kupata Takwimu yenye taarifa za Jumuiya zilizo hai ambazo ni sahihi,za kutosha na ambazo ni rahisi kuzipata.
Iwapo wewe ni Mwakilishi wa Jumuiya ya Kizanzibari ambayo imo kwenye Takwimu hii, tafadhali angalia Taarifa za Jumuiya yenu na zihakikishe data hizo katika ukurasa wa Jumuiya yenu kwamba ni za kweli.Iwapo umegundua makosa yoyote na ungependelea kurekebisha au iwapo unataka kuongeza Taarifa yeyote,bonyeza sehemu ya "Saidia Kurekebisha au Kukamilisha data/Taarifa"sehemu hii ipo Mwisho wa kurasa kwaajili ya kurekebisha Taarifa yako. Ombi lako la hilo la kurekebisha Taarifa litawasilishwa Wizara ya Utawala Bora,na kufanyiwakazi ipasavyo.
Iwapo Jumuiya yako haijaorodhweshwa kweye Takwimu hii, basi wawezapeleka Ombi la Kuingizwa. Ili kuingizwa kwenye Takwimu hii ni lazima Jumuiya yako iwe imesajiliwa chini ya Msajili Mkuu wa Zanzibar chini ya Sheria ya Usajili wa Vyama No 6 ya 1995.
Tahadhari:Iwapo uliwasilisha Dodoso lako ofisi za NGO Resource Centre baada ya tarehe ya Mwisho maombi Octoba 31, 2007,yawezekana kwamba maombi hayo yamepokelewa lakini hayakuingizwa kweye Takwimu hii.Njia ya Haraka ya kuingiza Taarifa zenu kwenye Takwimu hii ni Jaza Dodoso jipya kweye Mtandao.
Jumuiya zitazoingizwa kwenye Takwimu hii ni zile zilizosajiliwa na Msajili Mkuu wa Zanzibar chini ya Sheria No 6 ya mwaka 1995.Iwapo bado hujasajili Jumuiya yako Zanzibar,unaweza kusajili Jumuiya yenu nyinyi wenyewe katika Ofisi ya Mrajis Mkuu, iliopo Jumba la Mambo Msiige,Kelele Square,Shangani,Mji Mkongwe,Unguja.
Jumuiya ambazo hazijasajiliwa na Serikali ya Muungano au ya Zanzibar zinalazimika kupeleka Kopi mbili za Katiba ikiambatana na barua ya maombi kwa Msajili Mkuu.
Katiba yenu ni lazima ioane na muda uliopangiwa ukurasa wa 29 wa Sheria ya Vyama(Angalia chini).baada ya kipindi cha wiki mbili,wakilishi wenu lazima arudie Ofisi ya Msajili mkuu ili kuthibitisha maombi .iwapo maombi yamekubaliwa,Jumuiya yenu lazima ipeleke kopi tatu za ziada zenye kava ngumu(spiral binded) na ni lazima kulipia ada zote zinazohitajika.(Angalia chini kwa maelezo zaidi kuhusu Ada).Utaratibu wote huu unachukua si chini ya mwezi mmoja.
Jumuiya ambazo zimesajiliwa na Serikali ya Muungano na zinataka kufungua Ofisi zake hapa Zanzibar ni lazima ziwasilishe kopi tatu za Katiba zilizothibitishwa,kopi tatu za Usajili wao,na barua ya maombi kwa Msajili Mkuu Zanzibar.Vile vile iwapo Mkurugenzi wa Jumuiya kwa upande wa Zanzibar si Mtanzainia,hivyo basi Jumuiya italazimika kuwasilisha barua inayothibitisha uteuzi wa Mkurugenzi huyo kutoka Ofisi Kuu,na vilevile Jumuiya itapaswa kuwasilisha picha ya Mkurugenzi huyo kiwango cha Paspoti na C.V yake.Utaratibu huu wote unachukua si chini ya wiki tatu.
Ada zifuatazo zimeanza kutumika tangu mwezi wa December,2007.Kwa ada mpya unaombwa kuwasiliana na Ofisi za Msajili Mkuu moja kwa moja kwa anuani zao ziliopo hapo Chini.
Fomu za maombi: TSH 30,000/=
Ada ya Usajili: TSH 15,000/=
Fomu ya Bodi ya Wadhamini: TSH 2,000/=
Usajili wa Bodi ya Wadhamini TSH 15,000/=
Jumla: TSH 62,000/=
Fomu ya Maombi: TSH 40,000/=
Ada ya Usajili: TSH 15,000/=
Ada ya Usajili wa Bodi ya Wadhamini Fee: TSH 15,000/=
Ada ya fomu ya Maombi:TSH 4,000/=
Jumla: TSH 74,000/=
Fomu ya Maombi: 80$
Ada ya Usajili: 30$
Fomu ya Bodi ya Wadhamini: 10$
Ada ya Usajili wa Bodi ya Wadhamini: 300$
Maombi ya Fomu: 20$
Jumla: 440$
Simu ya ndani: +255 (0) 242 236324
Faksi: +255 (0) 242 236325
Baruapepe:
Sheria ya VYAMA namba 6 ya 1995, ukurasa namba 29
1. Jina la Jumuiya.
2. Madhumuni ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo
3.Watu ambao wanaruhusiwa kuwa wnachama
4. Bodi ya Wadhamini
5. Ada ya kujiunga na Jumuiya na Ada ya uanachama.
6. Taratibu za kumsimamisha au kumfukuza mwanachama.
7. Vyeo vya Maofisaa,ofisi zao,taratibu za Uchaguzi,kuteuliwa,kufukuzwa au kusimamishwa.
8. Kamati ziliopo(kama zipo)za Jumuiya,Sheria zinazowawajibikia maofisa wa kamati hizo,utaratibu wa uchaguzi,uteuzi,kusimamishwa na kufukuzwa.
9. Mamlaka na taratibu za kuziba nafasi za kazi katika kamati.
10. Udhamini na Kuekeza Fedha na mali za Jumuiya, na Vyeo vya maofisa wanaohusika na suala hilo.
11. Madhumuni ambayo Fedha za Jumuiya zinaweza kutumika
12. The inspection of the books and names of members by any member or officer, pursuant to subsection (1) of section 25 of this Act.
13. Taratibu za Mikutano.